Imebobea katika ukadiriaji mahususi wa gharama kwa kazi za ujenzi, ikijumuisha mchanganuo wa gharama za ujenzi (BOQ), Bei za kujaza kwenye mikataba ya ujenzi (Zabuni), na makadirio ya vifaa vya ujenzi pamoja na gharama za ufundi.
Kutoa makadirio sahihi ya gharama ya kazi za barabara, inayojumuisha miradi mbalimbali kama vile barabara za kiwango cha lami, Barabara za changalawe, na matengenezo na ukarabati wa Barabara za changalawe, kuhakikisha kunapatikana makadirio sahihi.
Inatoa utaalam katika ukadiriaji wa gharama kwa kazi za ujenzi, katika makundi ya kazi za uhandisi wa Mabomba, Kazi za Umeme na TEHAMA.
Pata ufikiaji wa hifadhidata pana ya bei za soko za vifaa vya ujenzi kutoka kwa maduka ya vifaa vya ujenzi kote nchini Tanzania, kuwezesha kufanya maamuzi sahihi na ununuzi wa gharama nafuu kwa kulinganisha bei ya soko ya vifaa vya ujenzi bila kuzunguuka kutafuta maduka. Pia inatoa nafasi ya wamiliki wa maduka kutangaza maduka yao kupitia mfumo na kuwafikia wateja kirahisi.
Huduma za ushauri wa ukadiriaji gharama za ujenzi katika hatua ya ubunifu wa michoro na katika hatua ya usimamizi wakati wa ujenzi. Lengo letu ni kuhakikisha gharama za mradi zilizoboreshwa kupitia upangaji bajeti sahihi, ukadiriaji sahihi, ununuzi vifaa sahihi kwa kutumia programu yetu ya HALA BuildCostManage Software.